Alhamisi, Machi 30, 2017

SERENGETI BOYS YAIUA BURUNDI KWA 3-0

Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 Serengeti Boys wamefanikiwa kutumia vema uwanja wa nyumbani Kaitaba, mkoani Kagera baada ya ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Vijana wenzao wa timu ya taifa ya Burundi chini ya miaka 17.
Serengeti Boys wamekutana na vijana wa Burundi katika mechi ya kirafiki ikiwa ni moja ya maandalizi ya kwenda kupambana katika kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri wa chini ya miaka 17 nchini Gabon yatakayopigwa hivi karibuni.
Magoli katika mechi ya leo yamefungwa na Muhsin Makame dk 20, Nickson Kababage dk 38 na Yohana Nkomola dk 72. Vijana hawa wa Tanzania na Burundi watakutana tena siku ya jumamsi watakaporudiana katika uwanja huo wa Kaitaba mkoani Kagera.

0 comments:

Chapisha Maoni