Jumatano, Machi 15, 2017

RIPOTI: MUELEKEO WA UCHUMI WA TANZANIA NI MZURI

Ripoti iliyotolewa mjini Dar es salaam na Kampuni ya Exotix ya Uingereza ikishirikiana na Benki ya Equity Investment, inaonyesha kuwa uchumi wa Tanzania una mwelekeo mzuri.
Ripoti hiyo inasema sehemu kubwa ya kutofanya vizuri kwa sekta ya benki na madhara yake kwa sekta binafsi, kunatokana na hatua za Rais John Magufuli wa Tanzania kupambana na ufisadi na ukwepaji wa kodi, ambako kwa muda mfupi kumeonekana kukwamisha uchumi, lakini kwa baadaye kutakuwa na manufaa ya muda mrefu.
Baadhi ya hatua zilizochukuliwa na Rais Magufuli ni kuwafukuza kazi baadhi ya wakuu wa idara muhimu za umma, kupambana na wafanyakazi hewa na kuchukua hatua nyingi za kubana matumizi.
Shirika la fedha la Kimataifa IMF limekadiria kuwa ongezeko la uchumi wa Tanzania kwa mwaka kati ya 2016 na 2021 litakuwa asilimia 6.7.

0 comments:

Chapisha Maoni