Jumatano, Machi 29, 2017

NAIBU MEYA IRINGA AHIMIZA MAADILI KWA VIONGOZI WA DINI

Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Mjini, Joseph Nzala Lyata (Chadema) amewataka wachungaji wa makanisa kutokalia kimya vitendo vya ukiukwaji wa maadili na kukemea vitendo vya viongozi wa kidini kujivika vazi la Umungu ilihali matendo yao yameegemea katika uasi.
Naibu Meya ameyasema hayo akiwa katika kanisa la Lutheran K.K.K.T Iringa mjini jumapili iliyopita alipomwakilisha mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa katika uzinduzi wa Albamu ya kwaya iitwayo 
Mhimidini.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Lyata ametoa mifano ya tabia za ukiukwaji wa kanuni za kidini kwa viongozi kuwa ni pamoja na kushindwa kuwa mfano bora kwa waumini wanaowaongoza na kuishi maisha ambayo wamekuwa wakiyahubiri katika madhabahu mbalimbali.
Katika uzinduzi huo Lyata pia aliongoza harambee ya shilingi milioni 15 na kufanikiwa kupatikana kwa shilingi 2,500,000 zilizokusanywa hadi sasa.

0 comments:

Chapisha Maoni