Jumatano, Machi 29, 2017

MAJINA 12 YA WAGOMBEA UBUNGE EALA KUTOKA CCM HAYA HAPA +VIDEO

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza majina 12 ya makada wake ambao watawania kuteuliwa ili waweze kuwa wawakilishi kwenye Bunge la Afriika Mashariki (EALA).
Akitangaza majina hayo mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za CCM jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa, miongoni mwa waliyoteuliwa; makada 8 ni kutoka Tanzania Bara na 4 kutoka Zanzibar.

“Katika mchakato wa kuwapata wawakilishi wa chama kwenye uteuzi wa wabunge wa EALA, tulitoa matangazo, tukapata wana CCM 450 walioomba kupewa ridhaa hiyo ya kuiwakilisha nchi kwenye Bunge la Afrika Mashariki. Miongoni mwao wanawake ni 93 na wanaume ni 357 ambao wote walipita kwenye michujo tukapata majina haya 12.”
“Mchakato unaofuata ni kuyapeleka majina haya 12 Bungeni Dodoma ili yakapewe ridhaa na bunge, watakaoshinda ndiyo watakuwa wawakilishi wetu EALA.”
“Chama kinawapongeza wale wote waliopata uteuzi na ambao wamekosa, tuendelee kushikamana na kukijenga chama chetu pamoja na nchi yetu.” Alisema Polepole.

Waliopata uteuzi

Bara

Wanawake

Zainab Rashid Mfaume Kawawa
Happiness Elias Lugiko
Fancy Haji Nkuhi
Happiness Mgalula

Wanaume

Dkt. Ngwalu Jumanne Maghembe
Adam Omary Kimbisa
Isey Macha
Charles Makongoro Nyerere

Zanzibar

Wanawake

Mariam Yusi Yahya
Rabia Abdallah Hamid

Wanaume

Abdallah Hasnu Makame
Mohammed Yusuf Nuhu

0 comments:

Chapisha Maoni