Jumatano, Machi 29, 2017

HATIMAYE RC MAKONDA MBELE YA KAMATI YA MAADILI BUNGENI DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amefika mbele ya Kamati ya Maadili Haki na Madaraka ya Bunge.
Taarifa ya kamati itafikishwa kwenye Bunge zima na kusomwa.
RC Paul Makonda aliwasili Bungeni na kupokelewa na Mkuu kitengo cha Habari-Bunge Owen Mwandumbya kuitikia wito wa Kamati ya Bunge.
RC Makonda ameitwa kujibu tuhuma za kutoa matamshi ya kudharau Mamlaka ya Bunge aliyotoa mapema mwaka huu kwamba wengi wao hakuna wanachofanya zaidi ya kuchekesha na kulala tu bungeni.
Ikumbukwe kuwa Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo, Harisson Mwakyembe amesema hawezi kuwasilisha taarifa ya upande mmoja na isiyokamilika sakata la uvamizi Clouds na kwake jambo hilo sio kipaumbele wizarani.
Amesisitiza yeye kama mwanasheria anaheshimu kanuni za asili(Principles of natural justice) kwa kusikiliza upande wa pili.

0 comments:

Chapisha Maoni