Mahakama ya Haki ya Ulaya (ECJ) yenye makao yake
huko Luxembourg jana Jumanne ilipasisha marufuku ya vazi la staha la
mwanamke wa Kiislamu, hijabu.
Kwa mujibu wa hukumu ya mahakama hiyo, waajiri wa Ulaya
wanaweza kuwazuia wafanyakazi wao kuvaa nembo za kidini likiwemo vazi
staha la hijabu.
Hii ni hukumu ya kwanza kutolewa na mahakama ya Ulaya kuhusu mjadala
wa vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu, hijabu katika maeneo ya kazi.
Mahakama ya Haki ya Ulaya iliyochunguza mafaili na matukio ya kufutwa
kazi wanawake wawili wanaovaa vazi la hijabu katika nchi za Ubelgiji na
Ufaransa imetangaza kuwa, ni haki ya kisheria ya kila shirika na kampuni
kuwataka wafanyakazi wao kuwa na muonekano usioegamea upande wowote
wala kuwa na alama za kidini, na mahakama hiyo imeruhusu mashirika
kuzuia alama na nembo za kisiasa, kifalsafa au kidini.
Hukumu hiyo ya mahakama ya Ulaya ya ECJ kwa hakika imetolewa kwa
shabaha ya kuzuia vazi la staha la wanawake wa Kiislamu, hijabu
wanaofanyakazi katika makampuni na taasisi mbalimbali za Ulaya. Hatua
hii si tu kwamba ni ubaguzi wa wazi dhidi ya wanawake wa Kiislamu, bali
pia imewapa mamlaka makubwa waajiri kutumia hukumu hiyo kwa ajili ya
kuwabana zaidi wafanyakazi wa kike Waislamu na kuwapa hiari ya ama kuvua
mavazi yao ya hijabu au kufutwa kazi.
0 comments:
Chapisha Maoni