Ripoti mpya iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha
kuwa idadi ya wafungwa wanaoshikiliwa katika jela za Marekani ni kubwa
zaidi kuliko ya nchi zote duniani na hivi sasa kuna karibu wafungwa
milioni mbili na laki tatu katika jela za nchi hiyo.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa
idadi ya wafungwa walioko katika jela za Marekani ni mara tano zaidi ya
idadi ya wafungwa wa nchi zenye wafungwa wengi duniani. Kwa mujibu wa
ripoti hiyo, idadi ya wafungwa wahajiri huko Marekani pia imeongezeka.
Imebainika pia kwamba kati ya kila wafungwa watano walioko katika jela
huko Marekani, mfungwa mmoja amehukumiwa kifungo jela kwa kosa
linalohusiana na madawa ya kulevya.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa kuna haja ya
kutazamwa upya sera ya kuendesha mapambano dhidi ya mihadarati ili
kukomesha kuwepo idadi kubwa kama hiyo ya wafungwa nchini Marekani, bali
pia liangaliwe upya jibu la jamii ya Marekani kuhusu vitendo vya
utumiaji mabavu.
Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya "Policy
Think Tank" kuhusu wafungwa imeashiria pia kuhumiwa vifungo vya jela
watoto 6,600 huko Marekani na kubainisha kuwa watu wasiopungua elfu 57
wamefungwa jela huko Marekani kwa sababu tu ya kuingia nchini humo.
Aidha inatarajiwa kuwa siasa dhidi ya wahajiri za Rais Donald Trump wa
Marekani zitapelekea kuongezeka idadi ya wahajiri watakaofungwa jela
nchini humo.
Huwa napitia hapa kwa kuangalia kinachoendelea hapa....duniani!!
JibuFuta