Jumanne, Machi 21, 2017

LEO NI SIKU YA MAJI DUNIANI, VIJIJINI BADO CHANGAMOTO


Wakati dunia ikiazimisha siku ya kimataifa ya maji hii leo imeelezwa kuwa hakuna mabadiliko makubwa yaliyotokea katika upatikanaji wa maji nchini Tanzania, hususani katika maeneo ya vijijini, katika kipindi cha miaka kumi iliyopita
Umoja wa mataifa unahimiza uhakika wa maji safi na salama kupitia Lengo la sita la maendeleo endelevu linadhamiria kuona kuna upatikanaji wa maji safi na salama kwa wote ifikapo 2030.
Utafiti uliozinduliwa jana na taasisi ya twaweza umeeleza kuwa tatizo la upatikanaji wa maji lingali changamoto kubwa kwa jamii nyingi barani Afrika ambapo asilimia 38 ya wakaazi wa vijijini wanahitaji zaidi ya saa zima kupata maji.

0 comments:

Chapisha Maoni