Timu ya soka ya Simba imefanikiwa kutangulia kwa jumla ya pointi 5 baada ya kuifunga Yanga mabao 2-1 uwanja wa Taifa Temeke, Dar es Salaam na kuendelea kukaa kileleni mwa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016-2017.
Ikiwa ni mechi ya pili kwa msimu huu kukutana watani hao wa jadi wenyeji wa Kariakoo jijini Dar, huku ikiwa ni mchezo wa raundi ya pili, winga Ramadhani Kichuya anaifanya Simba kuzima ubishi na tambo za mahasimu wao Yanga baada ya kufunga goli la pili dk 81 baada ya lile la kusawazisha lililofungwa na Laudit Mavugo dk 66. Hii ni baada ya bao la Msuva alilofunga kwa mkwaju wa penati dk 5 na kuifanya Yanga kuongoza mpaka dk ya 65.
Rekodi ya kadi nyekundu kwa watani hawa wa jadi katika mechi za ligi kuu imeendelea kuwekwa ikiwa ni mechi ya tatu mfululizo kwa Simba kucheza pungufu uwanjani baada ya beki Janvier Besala Bokungu kupigwa umeme dk 55.
Kikosi cha Simba SC walikuwepo Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga/Shiza Kichuya dk51, Abdi Banda, James Kotei, Ibrahim Hajib, Muzamil Yassin, Juma Luizio/Said Ndemla dk27, Laudit Mavugo na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Jonas Mkude dk57.
Upande wa Yanga kilikuwa na Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Andrew Vincent, Kevin Yondan, Justine Zulu/Juma Mahadhi dk78, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko/Said Juma ‘Makapu’ dk45, Amisi Tambwe/Deus Kaseke dk70, Obrey Chirwa na Haruna Niyonzima.
Baada ya mechi ya leo, Simba SC wanaendelea kuongoza ligi na jumla ya pointi 54 wakati watani wao Yanga wakisalia katika nafasi ya pili ya pointi 49.
0 comments:
Chapisha Maoni