Viongozi wa Tanzania mkoani Dodoma sasa wametoa wito kwa wakulima kufuga punda kwa wingi ili kunufaika na mahitaji ya juu ya nyama yake barani Asia.
“Hapo awali nyama ya punda haikuzingatiwa kama mlo, lakini sasa wakulima wanatakiwa kujua kwamba nyama ya punda ni mlo muhimu barani Asia,” Osumo Kipisi, afisa wa mifugo mjini Dodoma alisema.
Kando na nyama ya punda kuwa mlo maarufu barani Asia, viungo fulani vya ngozi yake pia hutumika kutengeneza dawa na bidhaa za kujipamba barani Asia.
Inakisiwa kuna punda 250,000 wanatumiwa kubeba mizingo na kufanya kazi zingine nchini Tanzania.
Kichinjio cha punda mjini Dodoma huchinja punda 150 hadi 200 kwa siku kwa mauzo ya nje nchini Uchina na Uturuki, na kupata hadi dola 200 kwa kila punda.
0 comments:
Chapisha Maoni