Mshambuliaji wa Manchesater United
Zlatan Ibrahimovic alifunga bao la ushindi dakika za mwisho na kumpatia
mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho kombe lake la kwanza tangu
ajiunge na klabu hiyo kwa kuishinda Southampton.
Southampton
walionyesha mchezo mzuri wakati wa mechi hiyo lakini wakavunjwa moyo na
uamuzi wa utata uliompa bao la ushindi raia huyo wa Sweden mwenye umri
wa miaka 35.
Mshambuliaji wa Saints Manolo Gabbiadiani alifunga bao lililokataliwa
kabla ya Manchester United kupata bao la pili kupitia Ibrahimovic
kunako dakika 19 kabla ya Jesse Lingard kufunga ikiwa imesalia dakika
saba mechi kukamilika.
Southampton ilifunga mabao yake mawili kupitia Gabbiadiani katika vipindi vyote viwili vya mechi.
Oriel Romeu alipiga mwamba wa goli kabla ya Ibrahimovic kufunga kupitia
krosi iliopigwa na Anders Herrea dakika tatu kabla ya mechi kukamilika
na hivyobasi kuipatia ushindi Manchester United.
0 comments:
Chapisha Maoni