Serikali ya Burundi imeamua kususia mazungumzo ya Arusha yaliyopangwa kuanza leo hadi jumamosi (Februari 16 hadi 18) kwa lengo la kutatua mgogoro wa kisasa ulioanza mwaka 2015.
Msemaji wa serikali ya Burundi Bw Philippe Nzobonariba amesema serikali ya Burundi haitatuma wajumbe kwenye mkutano huo kutokana na kujitokeza kwa dosari kwenye kuwaalika washiriki wa mkutano huo.
Amesema warundi wanahitaji mshikamano wa kimataifa, lakini pia chaguo lao kuhusu mchakato wa mazungumzo linatakiwa kuheshimiwa.
Bw Nzobonariba amelalamika kuwa baadhi ya makundi yaliyoalikwa si vyama vya siasa vilivyosajiliwa na wizara ya mambo ya ndani ya Burundi, na mjumbe wa Umoja wa mataifa aliyealikwa alipingwa na serikali ya Burundi mwezi Desemba mwaka jana.
0 comments:
Chapisha Maoni