Jumamosi, Aprili 02, 2016

WAFANYAKAZI 600 WA KENYA AIRWAYS KUPIGWA KALAMU NYEKUNDU!

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways limetangaza mpango wa kuwaachisha kazi wafanya kazi 600 kuanzia Mei mwaka huu ili kuzuia shirika hilo kuporomoka. Kwa mujibu wa afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo Bw Mbuvi Ngunze, shirika hilo limekuwa likishuhudia hasara na hatua hiyo inalenga kulifanya lishindane kikamilifu na kuanza kupata faida. Amesema shirika hilo ambalo limegubikwa na madeni pia litaangalia upya operesheni zake ikiwemo safari zake na muundo mzima wa kifedha.Wafanya kazi hao ni kutoka idara mbali mbali za kampuni hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni