JESHI la Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekamata Marobota
10 ya vitenge na Katoni 17 za Pampers pamoja na Gari lililotumika
kubebea hitu hivyo katika eneo ya Gezaulole lililopo pembezoni mwa
ufukwe wa bahari ya Hindi.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa kukamatwa kwa
gari lenye vitu hivyo ni mara baada ya kupewa taarifa na Raia wema kwa kuwa katika eneo hilo kunapitishiwa mali zisizotolewa ushuru.
Siro amesema kuwa Gari lililo kamatwa na Vitenge na Pampers ni aina ya
Suzuki Carry lenye namba za usajili T490 CQB ambalo nalo linashikiliwa
na Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam.
Pia Sirro amesema kuwa mwananchi anaeona kuwa alitelekeza gari hilo lililo na vitu hivyo ajisalimishe Polisi ili apelekwe Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) akalipie ushuru wa vitu hivyo.
Pia Sirro amesema kuwa mwananchi anaeona kuwa alitelekeza gari hilo lililo na vitu hivyo ajisalimishe Polisi ili apelekwe Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) akalipie ushuru wa vitu hivyo.
0 comments:
Chapisha Maoni