Maduka yanayomilikiwa na raia wa kigeni nchini Afrika Kusini jana (Jumapili) yaliporwa na wenyeji katika mtaa wa mabanda wa Natalspruit, mashariki ya Johannesburg huku kukiwa na hofu ya kuzuka upya kwa mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni nchini humo.
Mvutano ulianza pale wenyeji walipoanza kushambulia raia wa kigeni ili kulipiza kisasi mauaji ya wenyeji wawili huku wakidai kuwa mauaji hayo yalitekelezwa na raia wa Pakistan. Wenyeji walioonekena kughadhabishwa walifukuza raia wa kigeni na kupora maduka yao. Maafisa wa usalama walitumwa katika eneo la tukio kutuliza hali.
Kisa hicho kimekumbusha wengi mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni yaliyoshuhudiwa Aprili mwaka uliopita na kupelekea kuuawa kwa raia wengi wa kigeni huku maelfu wengine wakifukuzwa makwao.
0 comments:
Chapisha Maoni