Magaidi walishambulia mji mkuu wa Uturuki, Ankara siku ya Jumapili kwa mara ya pili katika kipindi cha mwezi moja, na kuua watu wasiopungua 34 na kujeruhi wengine 125 , kwa mujibu wa waziri wa afya wa Uturuki.
Mamlaka imesema kuwa gari ambayo ilikuwa imebeba bomu, iligonga basi karibu na bustani ya Guven ambayo iko katika jiji wa Ankara, na kusababisha mlipuko.
Majeruhi wanatarajiwa kuongezeka kwani mashambulizi yalitokea katika eneo lililo karibu na kituo cha basi na gari moshi ambapo watu wengi utembea kufanya manunuzi na kula chakula katika maduka na migahawa.
Awali, ubalozi wa Marekani, ilikuwa imetoa onyo maalum kwa ajili ya eneo hilo siku ya Ijumaa, na kushauri raia wake kukaa mbali na eneo la mlipuko.
0 comments:
Chapisha Maoni