Jumatatu, Machi 14, 2016

WANAUME WENYE MATATIZO YA UZAZI WANAKABILIWA NA KISUKARI, MIFUPA DHAIFU

Wanaume wenye matatizo ya uzazi wako kwenye hatari ya kupatwa na magonjwa kama kisukari na pia mifupa dhaifu baadaye katika maisha yao, hii ni kwa mujibu ya utafiti uliofanywa na wanasayansi wa chuo kikuu cha Skane nchini Sweden.
Kulingana na utafiti huo, wanaume wengi chini ya miaka 50 wanaotatizika kupata watoto walipatikana na viwango vya chini vya homoni ya “testetorone” ambayo ni homoni muhimu inayochangia kuwepo kwa nguvu za uzazi na pia misuli, uzito wa mifupa na kumea kwa nywele mwilini. Wanaume 192 walishiriki kwenye utafiti huo.

0 comments:

Chapisha Maoni