Jumatatu, Machi 14, 2016

KISA NINI NDEGE ASIUAWE KATIKA NYAYA ZA UMEME?

Umeme unaotumika majumbani kwetu una nyanya mbili, moja ina moto na nyingine haina moto. Umeme unaopita kwenye nyaya za Tanzania ni voti 230. Kama mtu akigusa nyaya mbili, au waya wenye moto na ardhi kwa wakati mmoja, tofauti ya shinikizo la umeme kati ya pande mbili itasababisha mkondo wa umeme kupita mwili wake, na anaweza kuumia au hata kufa. Lakini ni kwanini ndege wanagusa nyaya hizo bila kuumia? Ni kwa sababu anasimama kwenye waya mmoja tu, mkondo wa umeme hautapita mwili wake.
Lakini kama ndege akisimama kwenye waya wenye shinikizo kubwa sana, tofauti ya shinikizo la umeme kati ya miguu yake miwili itasababisha umeme kupita mwili wake na kumdhuru?
Tofauti ya shinikizo la umeme iko kati ya miguu yake, lakini ni dogo sana, hivyo ni umeme mdogo sana unaopita mwili wake, hivyo hautamdhuru hata kidogo.

0 comments:

Chapisha Maoni