Jumatano, Machi 09, 2016

UN KUKOMESHA NDOA ZA UTOTONI

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne (Jana) yalitangaza mpango mpya wa kuendeleza jitihada katika kukomesha ndoa za utotoni ifikapo mwaka 2030 na kulinda haki za mamilioni ya wasichana wanaoishi katika mazingira magumu duniani kote.
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) na shirika la Idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) yalitangaza mpango huo katika Siku ya Wanawake Duniani kama sehemu ya jitihada za kimataifa za kuzuia wasichana kuolewa wakuwa wadogo na kuwapa msaada wasichana ambao tayari wameolewa katika nchi 12 barani Afrika, Asia na
Mashariki ya Kati,ambazo zimeathirika kutokana na ndoa za utotoni.
Mpango huo mpya,unaojulikana kama Mpango wa Kimataifa wa UNFPA-UNICEF wa kuharakisha Hatua ya Kukomesha ndoa za utotoni,utahusisha familia,jamii,serikali na vijana kwa lengo la kukomesha ndoa za utotoni katika miaka 15 ijayo,taarifa kutoka vyombo vya habari ilisema.
"Kuchagua wakati na nani atakayekuoa ni moja ya maamuzi muhimu maishani,"mkurugenzi mtendaji wa UNFPA, Babatunde Osotimehin, alisema katika taarifa ya habari na kuongeza kuwa "Ndoa za utotoni zinanyima mamilioni ya wasichana nafasi hii."

0 comments:

Chapisha Maoni