Jumatano, Machi 09, 2016

MCHEZO WA COMPUTER (GAME) UTAKAOKUSAIDIA KULA CHAKULA BORA

Watafiti wa Uingereza wamebuni mchezo mmoja wa kompyuta ambao unaweza kuwasaidia wachezaji kubadilisha tabia yao ya kula chakula kisicho cha kiafya.
Mchezo huo ulibuniwa na watafiti wa chuo kikuu cha Exeter na chuo kikuu cha Cardiff. Nadharia ya mchezo huo iko katika msingi wa “Mafunzo ya Ubongo”, mchezo huo utaonesha picha za chakula cha aina mbalimbali, ambao unamtaka mchezaji kubonyeza wakati wa kuangalia picha za chakula kisichofaa kwa afya yake. Baada ya muda kadhaa, wachezaji watazoea kukataa wakati kuona chakula kisicho cha kiafya.
Watafiti waliwafanya watu 41 kujiunga na jaribio hilo, wengi wao ni wanene wa kupita kiasi ambao pia wana tabia ya kula chakula chenye kalori ya juu. Katika muda wa wiki moja, walitakiwa kucheza mchezo huo kwa mara nne, kila mara dakika 10.
Matokeo yanaonesha kuwa katika wiki hiyo, unene wa wastani wa watu hao ulipungua kwa kilogramu 0.7, kila siku wanapungua ulaji wa chakula chenye kalori 220.
Watafiti wamesema, ingawa mchezo huo unatakiwa kujaribiwa zaidi, asilimia 88 ya washiriki walisema wanapenda kuendelea kushiriki kwenye utafiti huo.

0 comments:

Chapisha Maoni