Alhamisi, Machi 10, 2016

18 WAFA AJALINI SINAI

Takriban watu 18 walikufa kutokana na ajali ya barabarani kusini mwa Sinai siku ya jumatano usiku,kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya ndani ya Misri.
Ajali hiyo ilitokea baada ya basi la kubebea abiria aina ya microbus kugongana na lori katika barabara Abu Rdees-Al-Tur kusini mwa Sinai,na watu 18 wakaaga dunia na miongoni mwao kulikuwa na polisi 12 na wanafunzi wanne.
Ajali za barabarani zimeathiri nchi ya Misri na kila mwaka takriban watu 12,000 huaga dunia kutokana na ajali hizo,taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani ilisema.

0 comments:

Chapisha Maoni