Watu watano wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya kushambuliwa na watu wawili kwa njia ya risasi katika jimbo la Pennsylvania, Marekani, siku ya Jumatano.
waathirika hao walikuwa wanaendelea na mbwembwe za sherehe waliposhambuliwa, katika mji wa Wilkinsburg, kilomita 13 mashariki mwa Pittsburgh.
Watu wanne waliuawa papo hapo na mmoja hospitalini alipokuwa anaendelea na matibabu.
Mkuu wa polisi katika eneo alisema watuhumiwa hao wawili walitoroka baada ya kutekeleza shambulizi hilo na msako dhidi yao unaendelea.
0 comments:
Chapisha Maoni