Jumatano, Machi 16, 2016

ULIJUA KUWA PLASTIKI HAIOZI?? HIVI NI VIJIDUDU VINAVYOOZESHA PLASTIKI

Plastiki ni uvumbuzi muhimu ambao pia umeleta usumbufu mkubwa. Bidhaa za plastiki zimerahisisha maisha ya binadamu, lakini takataka za plastiki ni vigumu kushughulikiwa. Mwaka 2010 nchi 192 zinazopakana na bahari zilitoa tani milioni 275 za takataka za plastiki. Takataka hizi zisizooza kwa urahisi zina athari mbaya kwa mazingira na viumbe.
Wataalamu wa biolojia wametupia macho vijidudu ili kujua kama vinaweza kuozesha plastiki kama vinavyoozesha majani. Hivi karibuni mwanasayansi a Chuo Kikuu cha Uhandisi cha Kyoto Prof. Kohei Oda na kikundi chake wamegundua vijidudu vyenye uwezo huo.
Prof. Oda alifikiri vijidudu hivi huenda viko katika sehemu zenye takataka nyingi za plastiki, hivyo yeye na wenzi wake walikusanya sampuli 250 zikiwemo maji na udongo kutoka kituo kinacholimbikiza takataka za chupa za plastiki. Waliweka sampuli hizi pamoja na plastiki nyembamba aina ya PET. Katika chupa ya No. 46, plastiki ilianza kuoza. Watafiti waligundua vijidudu aina ya Ideonella sakaiensis. Inatumia vijidudu hivi wiki 6 kuoza kikamilifu plastiki nyembamba, muda huo ni mrefu sana. Lakini jambo muhimu zaidi ni kwamba utafiti huo umethibitisha viumbe vinabadilika kwa kasi zaidi ili kukabiliana na mabadiliko ya dunia. Plastiki ilivumbuliwa katika miaka 70 iliyopita, lakini sasa viumbe wamekuwa na uwezo wa kuiozesha.

0 comments:

Chapisha Maoni