Jumatano, Machi 16, 2016

FIFA YATUMBUA MAJIPU YA SOKA SOUTH AFRICA

Maafisa 3 wa shirikisho la soka la Afrika Kusini wamepigwa marufuku na Shirikisho la soka duniani FIFA kwa tuhuma za kupanga mechi.
Watatu hao ni pamoja na aliyekuwa rais wa shirikisho hilo Leslie Sedibe ambaye amepigwa marufuku ya miaka 5 na kupigwa faini ya dola elfu $20,245 .
Maafisa wengine waliopigwa marufuku ni Steve Goddard na Adeel Carelse, ambao waliwahi kuwa viongozi wa idara ya waamuzi katika SAFA.
Wawili hao wamepigwa marufuku ya miaka miwili kila mmoja.

0 comments:

Chapisha Maoni