Jumatano, Machi 16, 2016

TIBA MPYA YA KISUKARI

Watafiti nchini Australia wamegundua aina moja ya mafuta ndani ya mwili wa binadamu yanayoweza kutoa mchango mkubwa katika kinga na tiba ya ugonjwa wa kisukari.
Dkt Paul Lee kutoka Taasisi ya utafiti wa matibabu ya Garvan alitaka kujua kama mafuta ya kahawia yanaweza kuathiri kiwango cha sukari katika damu na kama tiba inayolenga mafuta ya kahawia itasaidia kudhibiti ugonjwa wa kisukari. Dkt Lee amesema, wamegundua kuwa kuna uwezekano wa uhusiano kati ya mafuta ya kahawia na mabadiliko ya kiwango cha sukari katika damu. 
Dkt Lee ameongeza kuwa utafiti huo umeyafanya mafuta ya kahawia kuingia katika mfumo wa tiba za ugonjwa wa kisukari.

0 comments:

Chapisha Maoni