Alhamisi, Machi 10, 2016

MFAHAMU MARK ZUKERBERG, HAAMINI KUWA MUNGU YUPO, UTAJIRI WAKE NA MENGINEYO

1. Mark Zukerberg ndiye mmiliki wa mitandao ya Facebook Whatsapp na Instagram,
2. Ana umri wa miaka 31, alivumbua mtandao wa facebook akiwa na miaka 20 tu. Baadae akanunua mtandao wa Whatsapp na mwaka 2012 kampuni yakeey ya Facebook ikanunua mtandao wa Instagram. Hivyo anamiliki mitandao yote mitatu.
3. Mark Zuckberg anaeshikilia rekodi ya dunia ya kuwa bilionea mdogo zaidi aliyoiweka akiwa na miaka 23 tu!
4. Mark Haamini kabisa kuwa kuna Mungu,
5. Hajawahi kumiliki TV! Maisha yake amekuwa akitumia computer tu.
6. Mara kadhaa amepigiwa kura kuwa mtu maarufu anaevaa vibaya zaidi duniani! Mara nyingi huvaa t-shirt na jeans au kaptura na sandals. Wengi huona kama vile hajijali.
7. Unaweza kumblock mtu yeyote facebook kasoro yeye tu! Ukiingia kwenye ukurasa wake option ya kumblock ipo lakini haifanyi kazi. Ukiclick "bloc" inakuambia error. Kwa kifupi huwezi kumblock. Ingia hapa http://web.facebook.com/zuck na ujaribu uone!.
8. Mwaka 2009 Mark alivaa tai kwa mwaka mzima kuonyesha ni jinsi gani mwaka huo ulikuwa serious. Baada ya hapo Mark hakuvaa tai tena unless kuwe na matukio maalumu.
9. Akiwa na miaka 13 tu Mark alitengeneza mtandao wa familia uliokuwa ukiziwezesha kompyuta kutumiana meseji ndani ya nyumba yao!
10. Kabla ya kuuita mtandao huu "Facebook" aliuita "Facemash" badae akabadili jina kuwa "Facebook"
11. Mwaka 2011 aliamua kutokula nyama yeyote mpaka awe amechinja mwenyewe!
12. Alimuoa mkewe (Priscilla) May 19, mwaka 2012 siku ambayo mkewe alikua anahitimu shahada yake ya udaktari (MD) kutoka Chuo Kikuu cha Carlifonia. Kwahiyo sherehe ya harusi ilienda sambamba na sherehe ya graduation kwa mkewe.
13. Aliacha shule akiwa na miaka 20 chuo kikuu cha Havard (drop out). Inadaiwa alikua akibishana na waalimu wake (maprofesa) ambao walimlazimisha kujibu kadri alivyofundishwa. Alipojibu kwa kadri ya uelewa wake alikosa japo anaamini alikua sahihi kujibu vile alivyojua sio vile alivyokariri.
14. Alimuoa Priscilla Chan mwaka 2012 baada ya kukaa naye kwenye mahusiano kwa miaka 10. Walikutana mwaka 2003 wote wawili wakiwa wanafunzi chuo kikuu cha Havard.
15. Kwa mujibu wa mtandao wa http://www.boston.com jumla ya utajiri wao ni dola Bil.35 (takriban shilingi Trilioni 80 ambayo ni sawa na bajeti ya Tanzania miaka mitano). Lackini pato lao kwa mwaka (annual income) linakua kwa kasi sana. Mwaka 2015 pato lao lilikua dola bilioni 12.
Yani makusanyo yao kuanzia January 1 hadi December 31 mwaka 2015 yalikua Dola bilioni 12 sawa na shilingi trilioni 25 za kibongo. Jiulize ww mwaka jana ulikusanya shilingi ngspi? Makusanyi ya Mark kwa mwaka jana ni makubwa kuliko bajeti ya Tanzania kwa mwaka mmoja. Yani pato la mtu mmoja linzaidi pato la nchi.!

0 comments:

Chapisha Maoni