Siku kama ya leo miaka 140 iliyopita mvumbuzi wa Kimarekani,
Alexander Graham Bell alivumbua simu na siku hiyo hiyo akafanya
mazungumzo ya kwanza ya majaribio ya simu na msaidizi wake, Thomas
Watson. Uvumbuzi huo wa simu ulileta mabadiliko makubwa katika vyombo
vya mawasiliano.
Bell alifaidika na uzoefu na majaribio ya wahakiki na wavumbizi
wengine katika kutengeneza chombo hicho cha mawasiliano ya haraka. Baada
ya hapo chombo cha simu kiliboreshwa na kufikia kiwango cha sasa kwa
kukamilishwa kazi iliyofanywa na Alexander Graham Bell.
0 comments:
Chapisha Maoni