Jumanne, Machi 01, 2016

MAZOEZI YASAIDIA KUKINGA MARADHI YA FIGO YANAYOSABABISHWA NA UGONJWA WA KISUKARI

Watafiti wa chuo kikuu cha Tohoku cha Japani wametangaza kuwa kupitia jaribio la wanyama, mazoezi ya muda mrefu yataboresha maradhi ya figo yanayosababishwa na ugonjwa wa kisukari.
Kutokana na uharibu unaoletwa na kiwango kikubwa cha sukari katika damu kwa mishipa ya damu ya figo, wagonjwa wengi wa kisukari watapata maradhi ya kisukari. Madaktari siku zote wanaona kuwa mazoezi yataweza kuboresha hali ya maradhi ya figo, lakini maoni hayo hayajathibitishwa na majaribo ya kisayansi. 
Katika jaribio hilo, watafiti hao waliwagawanya panya wanaopata ugonjwa wa kisukari kwa vikundi viwili. Panya wa kikundi kimoja wanafanya mazoezi kwa dakika 60 kila siku na siku tano kwa wiki, na wa kikundi kingine hawafanyi mazoezi. Baada ya miezi miwili, hali ya figo ya panya wanaofanya mazoezi iliboreshwa.
Watafiti wanasema, matokeo ya utafiti huo umethibitisha mazoezi kweli yanatoa mchango katika tiba ya maradhi ya figo yanayotokana na ugonjwa wa kisukari.

0 comments:

Chapisha Maoni