Jumanne, Machi 01, 2016

KENYA KUWASAKA SIMBA WALIOTOWEKA HIFADHINI

Maafisa wa KWS wameanza operesheni ya kutafuta simba wawili walioripotiwa kuonekana katika msitu wa barabara ya Ngong, mjini Nairobi, Kenya wiki moja tu baada ya simba wengine kutoroka kutoka mbuga ya taifa ya Nairobi.
Shirika la huduma kwa wanyamapori (KWS) limesema kwamba simba hao wawili ni miongoni mwa sita walioripotiwa kutoroka kutoka kwa mbuga ya taifa ya Nairobi, mwezi wa Februari 19, 2016 ambapo simba jike na mtoto wake walipatikana baadaye na kurejeshwa kwenye mbuga hiyo.
Simba hao walionekana na polisi wa trafiki, waliokuwa wakipiga doria katika barabara ya Southern Bypass, mwendo wa saa nne asubuhi, shirika la huduma kwa wanyamapori (KWS) limesema kupitia taarifa.

0 comments:

Chapisha Maoni