Jumanne, Machi 01, 2016

JE, UNAFAHAMU UKIANGALIA KIOO WAKATI WA KULA, UTAHISI LADHA YA CHAKULA NI NZURI ZAIDI?

Ukila peke yako au pamoja na wenzako, utahisi ladha ya chakula itakuwa na utofauti? Watafiti wa Japani wamegundua kuwa chakula kitakuwa kitamu zaidi, wakati unapokula na wenzako, hata ukila peke yako hukui unajiangalia kwa kioo.
Watafiti wa chuo kikuu cha Nagoya cha Japani walifanya jaribio la hisia kuhusu ladha ya chakula wakati wa kuangalia kioo. Walioshiriki kwenye jaribio hilo walikuwa wanaona chakula ni kitamu zaidi wakati wanapokula wakiangalia kioo. 
Kwa upande mmoja, walioshiriki kwenye jaribio hilo hawana tofauti kuhusu chumvi na sukari. Kwa upande mwingine, kikoo hakikuathiri hali ya moyo wa watu hao.
Watafiti wanaona kuwa hisia kuhusu ladha ya chakula inaathiriwa na mazingira na utahisia ladha nzuri zaidi ukikula pamoja na wengine. Kuangalia kioo wakati wa kula ni sawa na kula chakula pamoja na wengine, hivyo utajisikia ladha ni nzuri zaidi.
Miaka ya hivi karibuni, idadi ya wazee inaendelea kuongezeka, hivyo hali ya kula pekee kwa mzee pia inaibuka. Watafiti wanaona kuwa ugunduzi huo unawasaidia wazee kuepuka kupoteza hamu ya kula chakula na ukosefu wa virutubisho.

0 comments:

Chapisha Maoni