Taasisi ya mzio na maradhi ya kuambukiza ya Marekani imefadhili utafiti
mmoja ukionesha kuwa kula karanga kuanzia utotoni kutasaidia kupunguza
kwa kiasi kikubwa hatari ya mzio wa karanga. Taasisi hiyo inarekebisha
“Mwongozo wa utambuzi na udhibiti wa mzio wa chakula wa Marekani”, na
kushauri watoto wadogo kula karanga ili kukinga mzio.
Suala la mzio wa karanga linafuatiliwa zaidi siku hadi siku kwa miaka zaidi ya kumi. Taasisi hiyo iliwafadhili watafiti wa chuo kikuu cha London kufanya jaribio moja, ambalo liliwashirikisha watoto wachanga wenye umri wa miezi 4 hadi 11 wanaokabiliwa na hatari kubwa ya mzio wa karanga. Nusu ya watoto hao kila baada ya muda kadhaa walikula chakula kidongo chenye karanga, lakini watoto wengine hawakula karanga hata kidogo.
Matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa, kwa wale waliokula chakula chenye karanga kila baada ya muda kadhaa, hadi kufikia umri wa miaka 5 hatari ya mzio wa karango ilipungua kwa asilimia 81.
Utafiti mwingine ulionesha kuwa mkakati huo wa kukinga mzio wa karanga pia unafaa kwa mzio wa mayai.

0 comments:
Chapisha Maoni