Jumatatu, Machi 14, 2016

BIA MPYA YENYE PROTINI MAHSUSI KWAAJILI YA KUJENGA AFYA

Kwa wapenzi wa kujenga misuli, kunywa bia sio jambo zuri, lakini kampuni ya Chakula cha Misuli ya Uingereza kimebuni bia yenye protini nyingi ambayo inaweza kukidhi mahitaji ya wapenzi wa kujenga misuli.
Chupa moja ya bia hiyo ina protini gramu 21.8, ambayo ni sawa na steki moja. Bia hiyo ni chaguo bora la watu wanaojenga misuli, ambayo kiwango chake ni asilimia 3.6, lakini idadi ya kalori ni theluthi moja ya bia ya kawaida, na kabohaidreti ni asilimia 15 ya bia ya kawaida.
Mhusika wa kampuni hiyo Darren Bill alipohojiwa na vyombo vya habari alisema, kudumisha mtindo wa maisha unaofaa kwa afya ni vigumu, hasa wakati ukitaka kunywa bia pamoja na marafiki zako. Lakini sasa wamepata kinywaji mbadala cha bia ya kawaida, ambapo inamaanisha kuwa mtu yeyote hataona kunywa bia ni kosa.

0 comments:

Chapisha Maoni