Jumatatu, Machi 14, 2016

BAADA YA JINNA LAKE KUTOONEKANA KATIKA UTEUZI, ABBAS KANDORO AZUNGUMZA

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ni kati ya viongozi ambao hawakuonekana katika uteuzi mpya wa kwanza wa wakuu wa mikoa uliofanywa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 
Amezungumza na kutoa ya moyoni baada ya uteuzi huo: “Unajua kuna watu wakituona wanajua kwamba bado tupo kwenye ujana, Ndugu mtangazaji mimi nina miaka 66 sasa hivi, tayari umri umenitupa mkono katika nafasi hii.
“Haijanishtua kwa sababu wakati tunapewa hii mikataba tuliambiwa kabisa ukomo wa mkuu wa Wilaya ni miaka 60 na Ukuu wa Mkoa ni miaka 66, hivyo nmetimiza umri wangu kisheria na napenda nimshukuru Mh Rais kwa hili” Alisema Abbas Kandoro.
Mpaka kustaafu kwake, Kandoro amehodhi nafasi ya ukuu wa Mikoa katika zaidi ya Mikoa Sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Singida na Mbeya.
Baada ya uteuzi mpya, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala ndiye sasa atakauwa mkuu wa mkoa wa Mbeya.

0 comments:

Chapisha Maoni