Ijumaa, Februari 19, 2016

WAZIRI MKUU ALIVYOIBUKIA BANDARI YA TANGA BILA TAARIFA

Katika hali iliyovuta hisia za wengi, Meneja wa bandari ya Tanga Ndugu Henry Arika alijikuta katika wakati mgumu alipotakiwa kutoa maelezo juu ya manunuzi ya Tag 3 ambazo zilinunuliwa zikiwa used na kwa sasa hazifanyi kazi huku maelekezo aliyopewa ni kununua Tag 2 mpya.
Waziri mkuu amabaye alifika bandarini katika mtindo wa ziara za kushtukiza mara baada ya kuhudhuria msiba wa baba yake na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu.
Kwanza alikataa kukaribishwa katika ofisi ya Meneja wa bandari na kumtaka ampeleke moja kwa moja kwenye hizo Tag mbovu ambazo gharama yake haiendani na hali ya vifaa hivyo.
Huyu meneja wa bandari ya Tanga ndiye pia alihusika katika kashfa ya kutoa bure kwa makontena ya Mohamed Enterprises mwaka 2012 wakati huo akiwa meneja biashara wa bandari Dar es salaam.
Ambapo habari zinaelezwa kuwa Mohamed enterprises alimsaidia fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la wasabato Vituka,ambapo washiriki wa kanisa walikubali kuwa ni kweli asilimia 90 ya gharama ya kanisa hilo ambalo thamani yake inakadiriwa kuwa milioni 550 zilitolewa na Henry Arika, kanisa hilo eneo la Yombo Vituka Sigara.
Kwa taarifa za mmoja wa wafanyakazi wa bandari ya Tanga ambaye alidai kuwa anamfahamu Ndugu ARIKA tangu wakiwa bandari ya Dar es salaam alidai kuwa Arika ni mla rushwa mzuri na ana mali nyingi ambazo ni tofauti na kiwango chake cha mapato, ikiwemo gari sita, ambazo ni land cruiser prado, toyota rav 4, benz new model, toyota harrier, bus aina ya eicher mbili. Pia ana nyumba tano hapa jijini Dar es salaam ambapo mbili zipo Vituka.
Matumizi mabaya ya cheo chake ambapo mtoto wake wa kike aliyemaliza kidato cha sita mwaka juzi bila kuwa na ujuzi wowote kwa sasa ni afisa mwenye cheo kikubwa hapo Bandarini Dar es salaam.
Henry Arika hakupatikana kuthibitisha tuhuma hizi zilizototolewa na mmoja wa wafanyakazi wa bandari tanga ambaye alidai kuwa anamfahamu vizuri Msabato huyu Henry Arika ambaye ni Meneja wa bandari ya Tanga.
Pia ana urafiki mkubwa na wafanyabiashara wengi hali inayolalamikiwa na baadhi ya wafanyakazi kuwa inarahisisha ukwepaji wa kodi kwa kubadilisha aina ya mizigo iliyopo kwenye makontena.
Waziri Mkuu amemuagiza Meneja huyo kumuandikia taarifa kamili juu ya uzembe huo na ukiukwaji wa agizo la serikali lakini kitendo chake cha kwenda kinyume na utaratibu wa manunuzi wa serikali.
Itakumbukwa pia Meneja huyu wa bandari ya Tanga alikosoa waziwazi agizo la kubana matumizi kwa kuzuia safari zisizo za lazima wakati alipokutana na Mkuu wa mkoa wa Tanga mwezi Januari.

0 comments:

Chapisha Maoni