Waziri wa Ujenzi wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa ameagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, TCRA, kusitisha mara moja mkataba wa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa mamlaka hiyo, Elizabeth Nzagi, kwa kushindwa kusimamia ugungwaji wa kifaa cha kufuatilia mapato ya simu ya ndani katika mitambo ya kuchunguza mapato katika mitandao ya simu (TTMS).
Waziri Mbarawa amesema kutokufungwa kwa kifaa hicho kumeisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 400/= hivyo ameiagiza pia bodi hiyo ya TCRA kuwasimamisha kazi mara moja, Kaimu Mkurugenzi anayesimamia mfumo wa uhakiki na usimamiaji huduma za mawasiliano, mhandisi Sunday Richard na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Modestus Ndunguru ili kupisha uchugnuzi dhidi ya uhusika wao katika kusababisha kifaa hicho kutokufungwa.
Aidha, Waziri Mbarawa ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRCA, Ally Simba kwa kutokuwa makini katika utendaji huo huku akimwagiza kuhakikisha kuwa kifaa hicho kinafungwa ndani ya siku saba.
0 comments:
Chapisha Maoni