Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amewasimamisha kazi wakurugenzi wa Halmashari nne nchini kwa tuhumiwa za kutoa rushwa kwa maofisa wa ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ili kubatilisha hati chafu zilizopata halmashauri zao.
Wakurugenzi hao ni wa Halmashauri ya Manispaa ya Misenyi Kagera Elizabeth Kitundu, Halmashauri ya Nanyumbu Mtwara Mohamed Kesenge, wa Halmashauri ya Kilolo Iringa Luckson Pia na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita Abdalla Mfaume.
Wakati huo huo Simbachawene amemvua madaraka mkurugezi wa mji wa Tunduma Halima Mpita na kuagiza mamlaka zimsimamishe kazi kupisha uchunguzi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na kuwatumia watoto wake katika shuguli za Halmashauri na kuwalipa posho na kusababisha upotevu wa mapato.
0 comments:
Chapisha Maoni