Jumatano, Februari 17, 2016

KUTOKULA CHAKULA CHA ASUBUHI KUNAWEZA KUSABABISHA KUVUJA DAMU UBONGO

Timu ya watafiti ya Japani imegundua kuwa, watu wasiokula chakula cha asubuhi wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kuvuja damu katika ubongo kuliko watu wanaokula chakula cha asubuhi kila siku.
Watafiti wanaona kuwa kutokana na kutokula chakula cha asubuhi, shinikizo la damu litaongezeka na kuongeza hatari ya kusababisha damu kuvuja katika ubongo, hasa wakati wa asubuhi ambapo shinikizo kubwa la damu litaweza kusababisha hali hiyo kwa urahisi zaidi.
Kuanzia mwaka 1985 hadi 2010, watafiti kutoka chuo kikuu cha Osaka na kituo cha utafiti wa saratani cha taifa waliwachunguza wazee elfu 80 nchini Japani, kati yao 1,051 walipata tatizo la damu kuvuja kwenye ubongo na 870 walipata ugonjwa wa moyo.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kiwango cha watu wasiokula chakula cha asubuhi ni asilimia 136 ya wale wanaokula chakula cha asubuhi. 
Utafiti wa awali ulionesha kuwa kutokula chakula cha asubuhi pia kuna uhusiano na shinikizo kubwa la damu na ugonjwa wa kisukari.

0 comments:

Chapisha Maoni