Takriban watu 28 waliuawa na wengine 61 kujeruhiwa siku ya jumatano (Jana) katika mashambulizi ya bomu yaliyotokea katika mji mkuu Ankara ambayo yalikuwa yamelenga jeshi la Uturuki,naibu wa waziri mkuu na msemaji wa serikali ya Uturuki,Numan Kurtulmus,alisema.
Kurtulmuş alithibitisha kuwa mlipuko huo ulisababishwa na bomu lililokuwa limewekwa kwenye gari na ambalo lilikuwa limelenga magari ya kijeshi ambayo yalikuwa yamebeba wafanyakazi wa Jeshi,lakini alisema kuwa hadi kufikia sasa serikali haina taarifa yoyote ya watu waliotekeleza mashambulizi haya.
0 comments:
Chapisha Maoni