Kampuni ya kutengeneza magari aina ya Volkswagen imetozwa faini ya dola milioni 8.9 za Marekani nchini Mexico kwa ajili ya kuuza karibu magari 45,500 bila vyeti vinavyohitajika vya mazingira,shirika la mazingira nchini humo lilisema.
Katika vyombo vya habari,Mwanasheria wa Shirikisho la Hifadhi ya Mazingira (Profepa) alikashifu vikali Volkswagen kwa kuuza kimakusudi magari aina ya Audi, Bentley, Porsche, Seat na Volkswagen bila kutekeleza sheria za mazingira nchini humo.
Ukaguzi huo uliofanywa ulionyesha kuwa kampuni hiyo ilikuwa imeleta na kuuza magari 45,494 bila vyeti vilivyokuwa vimehitajika vinavyohusisha kanuni mbili rasmi za Mexico.
0 comments:
Chapisha Maoni