Alhamisi, Februari 18, 2016

BAADA YA INDIA, SASA NI ZAMU YA CHINA KUADABISHWA NA TEMBO

Mafisa wa wanyamapori kwa ushirikiano na polisi wa mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, wanamtafuta tembo mmoja ambaye amekuwa akisababisha uharibifu kwa kuharibu magari yaliyoegeshwa kando ya barabara kwa siku tatu sasa.
Siku ya Jumatatu alasiri, tembo huyo aliripotiwa kuharibu magari tisa katika barabara moja kuu maarufu kwa jina G213, afisa wa wanayamapori alisema.
Tembo huyo wa kiume kwa jina la utani,Bamboo Shoot Teeth tayari ameharibu takriban magari 20.
Kulingana na maafisaa wa wanyamapori, Bamboo Shoot Teeth, huenda ana hasira kutokana na kushindwa na tembo mwingine walipokuwa wakipigania tembo wa kike.

0 comments:

Chapisha Maoni