RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ameweka rekodi ya kuwa kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi kuongoza waangalizi wa uchaguzi miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki kwenye Uchaguzi Mkuu wa Uganda unaofanyika kesho Alhamisi, Februari 18, 2016.
Mwinyi ambaye Mei 8 mwaka huu atatimiza umri wa miaka 91, ameteuliwa kuwa Kiongozi wa Waangalizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwenye Uchaguzi Mkuu wa Uganda na sasa amepiku rekodi iliyowekwa na Arthur Moody Awori, aliyeongoza timu ya waangalizi wa jumuiya hiyo waliosimamia Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2015.
Awori ambaye amewahi kuwa Makamu wa Rais wa Kenya, alikuwa na umri wa miaka 88 wakati alipoteuliwa na EAC kuongoza waangalizi wa jumuiya hiyo kwenye uchaguzi huo wa Tanzania.
Taarifa kutoka nchini Uganda zinaeleza kuwa mzee Mwinyi amekuwa kivutio miongoni mwa waangalizi hao takribani 50 kutoka EAC kutokana na umakini na utimamu wa mwili na akili zake, ingawa umri wake unaonyesha vinginevyo.
0 comments:
Chapisha Maoni