Ijumaa, Februari 19, 2016

UTAFITI WAONESHA KUWA AFYA YA WAZEE WANAOPENDA KUCHEKA NI NZURI ZAIDI

Watafiti wa Japani wamegundua kuwa afya za wazee wanaopenda kucheka ni nzuri zaidi.
Watafiti wa chuo kikuu cha Tokyo na chuo kikuu cha Osaka walishirikiana kufanya utafiti uliowalenga wazee elfu 20 wenye umri wa zaidi ya miaka 65 nchini Japani na kuchunguza uhusiano kati ya kucheka na hali ya afya.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, katika maisha ya kila siku, asilimia 38 ya wanaume na asilimia 49 ya wanawake wanacheka kwa sauti kila siku, na asilimia 10 ya wanaume na asilimia 5 ya wanawake wanacheka mara chache na hata hawacheki kabisa.
Baada ya kuchunguza uhusiano kati ya kucheka na afya, kati ya wazee wasiopenda kucheka, wengi zaidi walijitathmini kuwa hali zao kiafya siyo nzuri.
Kwa mujibu wa utafiti wa awali, kiwango cha kujitathmini hali ya afya cha mtu mmoja ni chini zaidi, na afya yake itakuwa mbaya zaidi. Hivyo inamaanisha wazee wanaopenda kucheka, afya zao ni nzuri zaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni