Watafiti wa chuo kikuu cha Oregon cha Marekani wamegundua kuwa, mboga za jamii ya kabichi zina viini lishe vinavyoitwa sulforaphen ambavyo vinaweza kuzuia ukuaji wa seli za saratani ya matiti.
Katika utafiti huo, wagonjwa 45 wa saratani ya matiti walifanyiwa utafiti kwa kutumia placebo na kuwafanya wengine kutumia dawa za sulforaphen. Sulforaphen iliyoko ndani ya dawa hizo ni kama kikombe kimoja cha brokoli.
Matokeo ya utafiti huo yanonesha kuwa matumizi ya sulforaphen yanapunguza kiwango cha ukuaji wa seli za saratani. Kula mboga nyingi za jamii ya kabichi ikiwemo brokoli, koliflawa na kabichi kunasaidia kupunguza kiwango cha kupata saratani ya matiti kwa wanawake.
0 comments:
Chapisha Maoni