Jumatatu, Februari 22, 2016

UKOSEFU WA USINGIZI WA MUDA MREFU UNAWEZA KUONGEZA HATARI YA KUPATA UGONJWA WA KISUKARI

Utafiti mpya unaonesha kuwa ukosefu wa usingizi wa muda mrefu unaweza kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari.
Watafiti wa chuo kikuu cha Colorado nchini Marekani wamesema, wamefanya uchunguzi kuhusu vikundi viwili ya watu 16 wenye umri wa miaka 20 hivi, watu wa kikundi cha kwanza walilala kwa muda usiozidi saa 5 kwa mfululizo wa siku tano, halafu wakalala kwa muda wa saa 9 kwa mfululizo wa siku 5. Na watu wa kikundi kingine walifanya kwa utaratibu wa kinyume.
Matokeo ya upimaji wa damu ya watu hao yanaonesha kuwa, watu wote walipolala kwa muda usiozidi saa 5, insulini mwilini mwao itapungua na kuathiri uwezo wa kudhibiti sukari. 
Mbali na hayo, utafiti wa awali uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard unaonesha kuwa wazee wanaolala kwa muda usiozidi saa 6 au unaozidi saa 8 wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa wa kisukari wa aina ya pili, na wanaolala kwa muda wa saa 7 hadi 8 wanakabiliwa na hatari ndogo zaidi. Inamaanisha kulala sana au chache si nzuri kwa afya.

0 comments:

Chapisha Maoni