Jumatatu, Februari 22, 2016

CHADEMA MBEYA WAVURUGANA, MWAMBIGIJA NA WENGINEO WAPIGWA CHINI

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji ya wilaya hiyo wamevuliwa uongozi kwa kile kilichodaiwa kuwapo kwa msuguano miongoni mwao.
Uamuzi huo ulifikiwa usiku wa kuamkia jana kwenye kikao cha mashauriano kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Zanzibar), Issa Said Mohamed.
Mohamed alipoulizwa kuhusu uamuzi huo, aligoma kulizungumzia kwa undani akidai hayo mambo ya ndani ya chama.
Hata hivyo, alikiri kusimamia kikao hicho ambacho kilianza saa 2.00 usiku na kumalizika saa 11.00 alfajiri.
Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki uliopo Maghorofani jijini hapa.
Taarifa za ndani ya chama zilizopatikana jana asubuhi, zilidai kuwa awali, wajumbe walimuomba makamu mwenyekiti huyo kufika jijini hapa na kuitisha kikao hicho kujadili msuguano uliopo.
Mmoja wa wajumbe waliokuwapo kwenye kikao hicho ambaye hakutaka kuandikwa mtandaoni, alisema kuliibuka malumbano makali huku wajumbe wakinyoosheana vidole kwa kutuhumiana.
Alisema wajumbe ndiyo wanaoharibu chama na kutengeneza makundi yasiyokuwa na tija.

0 comments:

Chapisha Maoni