Jumatatu, Februari 22, 2016

RAIS WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE AMEFIKISHA MIAKA 92

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alifikisha miaka 92 Jumapili (Jana) ambapo katibu mkuu wake,Misheck Sibanda,alisema kuwa kiongozi huyo mkongwe ambaye ametawala nchi hiyo tangu mwaka 1980,alikuwa bado katika udhibiti kamili wa serikali.
Misheck alisema kuwa Rais Mugabe katika umri wake bado ako na uwezo wa kufuata ratiba ya kila wiki kwa kina na akakashifu vikali uvumi unaoendelea nchini kwamba serikali inafanya kazi bila jitihada.
"Uvumi huu wote ni imani potofu kwa sababu Rais anafanya kazi na wakati mwingine yeye anafanya kazi hadi saa 9 usiku au 10 usiku,"Sibanda alisema katika mahojiano maalum ya gazeti la Jumapili la Mail.

0 comments:

Chapisha Maoni