Jumatatu, Februari 22, 2016

TANZANIA IKO MWISHONI KUTHIBITISHA DAWA MPYA YA KUTIBU KIFUA KIKUU (TB).

Wanasayansi kutoka taasisi ya kutafiti magonjwa ya Ifakara Health Institute (IHI) nchini Tanzania wanafanya majaribio ya mwisho ya kuthibitisha ubora wa dawa mpya ya kutibu ugonjwa wa kifua kikuu (TB).
Ikipitishwa, dawa hiyo inatarajiwa kupunguza muda ambao wagonjwa wa kifua kikuu wanameza madawa hayo kutoka miezi sita hadi chini ya miezi mitatu. Hii inatarajiwa kupunguza idadi ya wagonjwa wanaowacha kutumia madawa hayo kabla ya kumalizika kwa muda wa miezi sita kama inavyotakikana sasa.
"Kutakuweko na tiba mpya na bora zaidi ya TB nchini Tanzania na dunia nzima baada ya miaka mitano zijazo," Paul Smithson, afisa katika taasisi hiyo ya IHI alisema. Alisema kuwa itakapoidhinishwa, dawa hiyo mpya itakuwa na uwezo wa kutibu aina yote ya ugonjwa wa kifua kikuu.

0 comments:

Chapisha Maoni