Jumatatu, Februari 22, 2016

UNAPENDA VITU SUPER? SAMSUNG, ZTE NA HUAWEI WAMEZINDUA BIDHAA HIZI

Makampuni ya kutengeneza vifaa vya mawasiliano ya simu ya Samsung, ZTE na Huawei yalizindua bidhaa mbali mbali hapo jana (Jumapili) mbele ya kuanza kwa kongamano la Mobile World Congress (MWC) hivi leo jijini Barcelona, Spain.
Samsung ilizindua simu yake mpya ya Galaxy S7 huku ikijitahidi kudumisha ushawishi yake katika soko ya simu zinazotumia programu ya Android. Simu mpya za Samsung aina ya Galaxy S7 na Galaxy S7 edge zinakuja na teknolojia iliyoimarishwa kiasi cha kuziwezesha kuhimili vumbi na kuzama hadi futi tano ndani ya maji kwa muda wa dakika 30 bila kuharibika. Galaxy S7 ina skrini yenye upana wa inchi 5.1 huku Glalaxy S7 edge ikiwa na skrini yenye upana wa inchi 5.5.
Wakati huo huo Huawei ilizindua simu yake mpya kwa jina "MateBook". "MateBook" ambayo inatumia programu ya Windows 10 ina skrini yenye upana wa inchi 12 na unene wa milimita 6.9 pekee, kama ule wa iPhone 6. Simu hiyo ina betri inayohimili matumizi ya masaa kumi mfululizo.
Kwingineko ZTE ilizindua simu ya rununu iliyo na uwezo wa kutumika kama projector. Simu hiyo inakuja na betri ambayo itahimili matumizi ya masaa 10 ikiwa ina skrini yenye upana wa inchi 8.4.

0 comments:

Chapisha Maoni