Ijumaa, Februari 19, 2016

RWANDA NA TANZANIA ZAAHIDI KUBORESHA UHUSIANO

Serikali za Rwanda zimetangaza azma ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa pande mbili, kikanda na kimataifa na kuweka kando hitilafu zilizolemaza muamala wa pande mbili hizo katika miaka ya hivi karibuni.
Ahadi hiyo imetolewa wakati wa mkutano kati ya Rais Paul Kagame wa Rwanda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga mjini Kigali.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na Rais Kagame, Waziri Mahiga amesema Tanzania imeamua kufungua ukurasa mpya wa uhusiano na Rwanda kwa maslahi ya pande mbili na eneo zima la Afrika Mashariki. Mwanadiplomasia huyo wa Tanzania amesema mgogoro mashariki mwa DRC, hali ya hivi sasa nchini Burundi pamoja na changamoto za kiusalama katika eneo la Pembe ya Afrika vinahitaji ushirikiano wa kila nchi na kwamba Rwanda ni nchi muhimu katika kukabiliana na changamoto hizo.
Rais Kagame kwa upande wake amesema Jumuiya ya Afrika Mashariki haiwezi kufikia malengo yake endapo kutakuwa na hali ya kutoelewana miongoni mwa nchi wanachama.

0 comments:

Chapisha Maoni