Alhamisi, Februari 18, 2016

NGAZI ZINAZOPIGA MUZIKI WA PIANO

Ngazi zinazopiga muziki ya piano zimejengwa hivi karibuni katika duka kubwa mjini Shanghai China.
Ngazi hizi zimepambwa kama ni piano kubwa kwa kupakwa rangi nyeupe na nyeusi. Sensa za infrared zimewekwa kwenye kila ngazi, wateja wakipanda kila ngazi, itatoa sauti ya piano.
Ngazi hizi si kama tu zinawaburudisha wateja kwa muziki, bali pia zinawahimiza kufanya mazoezi kwa kupanda ngazi kwa miguu yao badala ya kupanda ngazi za umeme

0 comments:

Chapisha Maoni